Welcome to Mevity Company Ltd © 2026
Search

SEHEMU YA KWANZA: 1720 hadi 1973(KUTOKA KIJIJI CHA WAGENI, KUKALIWA NA WALIGOGO (Baadae Wagogo )HADI MAKAO YA BUNGE, KWA UFUPI )

Miaka mingi iliyopita mji huu ambao unaitwa Dodoma ulikuwa ukifahamika kama Calangu (Chalangu).

Kijiji hiki kilikua Sana na kuwa Mji mdogo wa Wageni mbalimbali. Mji huu haukuwa na wenyeji bali ulikuwa na wahamiaji toka maeneo mengine ambao ni wamanghala, wabambali, wayenzele na wanghulimba (Ambao baada ya muingiliano na Kuoana waliuunda Kabila la WAGOGO).Wahamiaji hawa walikuwa wakitofautiana kwa tabia zao, wamanghala na wabambali waliishi msituni(LEO hii ndio ambao wanahamia Sana Maeneo ya Mashambani) na walikuwa wawindaji wakila nyama na asali. Na wayenzele na wa wanghulimba walikuwa wakulima na wafugaji(Wapo Sana Upande wa Mashariki mwa Mkoa) .), Watu hawa (( wamanghala na wabambali, Wanghulimba na Wayenzele ) walikuwa waoga kiasili hivyo watu wengine walipoanza kuingia kutoka maeneo ya kaskazini wambugwe, magharibi wanyamwezi, Wasukuma na kusini wa wahehe watu hawa waliondoka na kwenda kuishi sehemu nyingine.

Sababu ya wahamiaji hawa kuitwa wagogo, inatokana na wafanyabiashara wakinyamwezi walipokuwa wakipita na bidhaaa zao kuelekea Pwani kwa biashara, walipofika kati ya Itigi na Manyoni walikuta mti mkubwa umeanguka na kuzuia njia, hivyo kwa muda mrefu wali lazimika kulala upande mmoja kabla ya kuvukia upande wa pili wa mti (gogo). Hii iliwafanya kila walipoulizwa wanalala wapi kabla ya kuendelea na safari walisema wanalala kwenye limgogo. Kwa sababu Calangu kilikuwa kijiji cha Wageni Mazungumzo mengi yalihusu Limgogo kama Uchawi na Maajabu ya kuwaka Moto, Mizimu ndimu baadhi ya Wenyeji wakajua wao ni LIMGOGO.Kwa hiyo wahamiaji hawa wakafahamika kama gogo (wagogo) kutokana na gogo hilo, Kipindi cha Ukoloni wa Ujerumani wakawa rasmi Wagogo badala ya Makabila ya hawali hapo juu.

Muingiliano wao ndio ulileta Wagogo. Mwaka 1907 Wajerumani waliweka makazi Calangu. Mnamo mwaka 1912 alifika mjerumani Dr. Spreling (Spelenje), na kuanzisha ngome yake, ngome hiyo kwa sasa ni ofisi ya Waziri Mkuu pale Mlimwa C.

Ofisi aliyokuwa akifanyia kazi za utawala na utoaji maamuzi kwa wahalifu (kufungwa, kuchapwa viboko na kunyongwa) kwa sasa ni Ofisi ya CCM Wilaya ya Dodoma Mjini pale Posta. Jengo la Wafungwa ndio Makao makuu ya CCM kwa sasa.Bustani aliyopenda kutembelea na kupumzika ilikuwa eneo la Kikuyu ambayo kwa sasa ni Chuo Kikuu cha St. John’s(Hlentch Garden )eneo hili kwa wakati huo lilikuwa tepetepe na mapitio ya wanyama watokao mbuga za kaskazini (Arusha) kuelekea mbuga za kusini (Mikumi). Mapitio ya wanyama hao ndio yaliyosababisha kubadilika kwa jina la eneo hili baada ya tembo kudidimia katika eneo hilo tepetepe karibu na shule ya sekondari mazengo ambayo sasa ni chuo kikuu cha St. Johns. Tendo hili la kudidimia kwa lugha ya Kigogo linajulikana kama IDODOMYIA hivyo baada ya kitendo hiki jina likabadilika kutoka Calangu (Chalangu) nakuwa Idodomia (DODOMA).

Mji wa Dodoma ulitangazwa rasmi kuwa makao makuu ya Chama na Serikali chini ya kifungu cha sheria No.320 ya mwaka 1973. Baada ya hapo matukio ya mafanikio yalifuata. Mwaka 1980 mji wa Dodoma ulipewa hadhi ya kuwa Manispaa. Mwaka 1995 serikali iliamua kuwa shughuli zote za bunge zifanyikie Dodoma. Bunge lilianza shughuli zake rasmi mwezi Februari 1996.

SEHEMU YA PILI: 1973 hadi 2026

Mwaka 1973, Serikali ya Tanzania chini ya Baba wa Taifa ,Mwl. Julius K. Nyerere ilitangaza kuhamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma. Baada ya hapo Msululu wa Matukio mbalimbali yalifanyika ili kukuza Dodoma.

TUKIO #1: KUUNDWA KWA CDA (Capital Development Authority): Aprili Mosi, 1978 Mamlaka ya Kukuuza na Kustawisha Makao Makuu (CDA) iliundwa ikiwa na Majengo makuu mawili:-

  • 1. Kukuza Uwekezaji mbalimbali Dodoma.
  • 2. Kupanga na Kusimamia Ukuaji wa Makao Makuu ya Nchi.

TUKIO #2: KUTANGAZWA KWA MANISPAA: Mwaka 1980, Dodoma ilitangazwa kuwa na hadhi ya Manispaa na kuvutia Uwekezaji mbalimbali kwenye Biashara, Viwanda na Majengo.

TUKIO #3: KUHAMIA KWA BUNGE LA TANZANIA: Mwaka 1995, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA lilitangazwa kuhamishiwa Dodoma na Mwezi Februari 1996 ,Bunge lilianza Rasmi Shughuli zake Dodoma. Dar Es Salaam bado ilikuwa sehemu muhimu ya Bunge ambapo baadae shughuli zote za Bunge zilihamia Dodoma.

TUKIO #4: JITIHADA ZA UWEKEZAJI MBALIMBALI NA SERIKALI: AWAMU YA KWANZA: Mwl. Nyerere aliweka Mkazo wa kiaminisha Watu hususani Serikalini na Nje and ya Serikali kuwa inawezekana kwa TANZANIA ikajitegemea na Kujenga Mji/Makao makuu yake bila hofu.

AWAMU YA PILI: Rais Ali Hassani Mwinyi alivutia Uwekezaji kwenye Biashara mbalimbali mfano Ujio wa Wahindi na kupewa Maeneo mbalimbali ili wafanye Biashara Ndio Mtaa wa Uhindini na Nyerere Square palikuwa na Soko kubwa la Biashara na Wahindi mpaka leo hii Wana maeneo pale Uhindini na walisaidia sana kuchangamasha Mji na Mzunguko wa Fedha.

AWAMU YA TATU: Rais Benjamin W. Mkapa aliweka malengo ya kuongeza Idadi ya Wakazi Dodoma kwa kuongeza Vyuo mbalimbali na Nyumba za Watumishi. Mfano Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma, Nyumba za Watumishi na Kugawa Ardhi bure kwa Watumishi ili Wahamie Dodoma na Wazaliane na Kuongezeka.

AWAMU YA NNE: Rais Jakaya M. Kikwete aliongeza Uwekezaji kwenye Ulinzi na Usalama wa Mji kwa kuongeza Vituo vya Jeshi, Ujenzi wa Makazi ya Wanajeshi, Shule za Sekondari na Vituo vya Afya n.k.

AWAMU YA TANO: Rais John P. Magufuli aliweka Mikakati ya kuhamia Rasmi kwa kuruhusu Wizara na Serikali ihamie Dodoma Mfano Kutangazwa kwa Dodoma kuwa Jiji, Ujenzi wa Mji wa Serikali n.k.

AWAMU YA SITA: Rais Samia Suluhu Hassani aliendelea na Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ya Kuwezesha Dodoma kuwa Makao Makuu mfano Uwanja wa Ndege wa Msalato, Mji wa Serikali, Ikulu, Barabara mbalimbali, SGR n.k.

TUKIO #5: UJENZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA: Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambacho kilianza Rasmi 2007 kilichangia mno kukua kwa Mji wa Dodoma kutokana na Idadi kubwa ya Wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali Tanzania pia Uchumi wa Maeneo Karibu na Chuo yalikua.Mfano Makulu, Ng'ong'ona, Iyumbu na Ntyuka. Pia kilichangia Ujenzi wa Nyumba za Watumishi kama Nyumba 300-Mwangaza n.k.

TUKIO #6: UJENZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA: TAMKO LA KUHAMIA DODOMA RASMI NA DODOMA KUWA JIJI Tamko la KUHAMIA DODOMA RASMI mwaka 2016 na Tamko la Dodoma kuwa Jiji yalibadilisha Mtazamo wa wengi kuhusu Dodoma na kuanza kuvutia Uwekezaji mbalimbali mfano;-

  • 1.Biashara
  • 2.Makazi na
  • 3.Kilimo na Ufugaji n.k.d

HITIMISHO: Historia ya Mji wa Dodoma ni pana na inayovutia. Kampuni ya MEVITY tulifanya Utafiti na kugundua mengi hususani Masoko ya Milki KUU hususani Nyumba, Ardhi na Majengo Mbalimbali. Karibu Upate Elimu Bure. Pia unaweza kutembelea tovuti yetu: mevity.co.tz ili kusoma Mwongozo wa Uwekeze.